HABARI NJEMA KUTOKA YANGA KUELEKEA MCHEZO DHIDI YA URA LEO - The Choice

HABARI NJEMA KUTOKA YANGA KUELEKEA MCHEZO DHIDI YA URA LEO

0

Uongozi wa klabu ya Yanga umeendelea kusisitiza kuwa hakuna tatizo baina yao na Mchezaji wa Kimataifa kutoka Zambia Obrey Chirwa na leo anatarajia kutua Zanzibar akiwa na Kocha Mkuu George  Lwandamina

Akizungumza nasi Mwenyekiti wa kamati ya Usajili na mjumbe wa kamati ya Utendaji Hussein Nyika amesema tatizo lililokuwa likimsumbua limekamilika kwani alikuwa anamatatizo binafsi .

” Alikuwa na matatizo binafsi sehemu aliyokuwa anaishi na mambo mengine alikuwa hajamalizia ila kwasasa kila kitu kipo sawa”

LWANDAMINA NA  CHIRWA KWENDA KWA PAMOJA ZANZIBAR LEO

Hussein Nyika  amesema kuwa Baada ya cHIRWA kumaliza matatizo yote yaliyokuwa yakimsumbua anatarajia kuelekea Zanzibar akiongozana na Mwalimu George ‘Chicken” Lwandamina.

VIPI ATACHEZA MCHEZO WA LEO?

Nyika amesema suala la kwenda Zanzibar ni leo ila kucheza au kutocheza litabaki kuwa suala la Kocha kama ataona inafaa kwa yeye kucheza au la.

Hata Hivyo katika moja ya taarifa ambazo tulikuwekea jana Kocha anayeiongoza Yanga katika michuano hiyo Shadrack Nsajingwa amesema hatarajii kutumia mchezaji mwingine nje ya wale ambao wapo kule Zanzibar.

Yanga itashuka dimbani leo kucheza mchezo wa nusu Fainali dhidi ya URA kutoka nchini Uganda katika mchezo unaotarajia kuanza majira ya saa kumi na robo kwa muda wa Afrika Mashariki,  tutakupa matokeo ya Moja kwa Moja kutoka uwanja wa Amani Zazibar.

1,186 total views, 4 views today

Facebook Comments
Share.

About Author