Haji Mwinyi agoma kuendelea na Yanga,awaandika barua ya kuomba kuondoka - The Choice

Haji Mwinyi agoma kuendelea na Yanga,awaandika barua ya kuomba kuondoka

0

MLINZI wa kushoto wa Mabingwa wa Tanzania Bara Dar Es Salaam Young Africans Maarufu kama Yanga, Haji Mwinyi Mngwali amefunguka mwenyewe kuhusiana na tetesi ambazo zimekuwa zikisemwa juu ya kutaka kuondoka kwake Yanga.

Haji Mwinyi ambaye amekuwa hapati nafasi ya kucheza mara baada ya Ujio wa Gadiel Michael Yanga msimu huu akitokea Azam Fc amefunguka Kila Kitu kuhusiana na Ishu Hiyo.

JE NI KWELI KAOMBA KUONDOKA

Haji Mwinyi  amesema ni kweli ameuomba uongozi wa timu ya Yanga ya JIJINI Dar Es Salaam aondoke kwenye klabu hiyo kutokana na kutopata nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha timu ya Yanga.

“Ni kweli nimeandika barua kwa Yanga ili kuangalia uwezekano wa mimi kutafuta timu nyingine nitakayopata nafasi ya Kucheza ”

NI TIMU GANI INAMWITAJI?

Haji Mwinyi ameitaja AFC Leopards ya nchini Kenya kuwa ndiyo timu inayomwitaji na imeshafanya naye mazungumzo huku Haji akisubiri barua kutoka Yanga ili kujua kama atakubaliwa.

“Mpaka sasa timu ambayo imefanya mazungumzo na mimi ni AFC LEOPARDS ya nchini Kenya, hata jana wamenipigia simu wakiniulizia kuhusu hii ishu nikawaambia nasubiri majibu kutoka kwa viongozi wangu (Viongozi wa Yanga)”

Share.

About Author