Home Michezo Haruna Niyonzima Atemwa Njee Na Simba Leo

Haruna Niyonzima Atemwa Njee Na Simba Leo

34
0
Kiungo wa Simba Haruna Niyonzima hatacheza mchezo wa fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup leo dhidi ya Gor Mahia kwa kuwa ana kadi mbili za njano.
Kulingana na kanuni za michuano hiyo, mchezaji mwenye kadi mbili za njano atakosa mchezo mmoja.
Kaimu Kocha wa Simba Masudi Djuma amesema ana wachezaji 18 hivyo kukosekana kwa Niyonzima hakuwezi kuwa tatizo.
Kesho Jumapili, Juni 10 2018, saa tisa Alasiri, Simba itashuka kwenye uwanja wa Afraha kumenyama na mapingwa watetezi wa michuano hiyo, Gor Mahia.