Haya ndio majibu ya mchezaji wa Simba, Ibrahim Hajib baada ya kufanya majiribio Misri - The Choice

Haya ndio majibu ya mchezaji wa Simba, Ibrahim Hajib baada ya kufanya majiribio Misri

0

Mchezaji wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Simba, Ibrahim Hajib ambaye hivi karibuni alienda Nchini Misri kufanya majaribio katika klabu ya Haras El Hodoud ya Ligi Kuu ya Misri.


Hajib (kushoto) akiwa na wachezaji wenzake wa Haras El Hodoud mazoezini leo mjini Alexandria

Hajib akiongea na Bin Zubeiry Sports kutoka mjini Alexandria yalipo makao makuu ya timu hiyo, Hajib alisema kwamba ameambiwa amefuzu majaribio yake baada ya siku tano.

“Nimepewa majibu kwamba nimefuzu, kwa hiyo kinachofuata ni hii klabu kuzungumza na Simba ili wakubaliane kwanza, ndipo nitajua mustakabali wangu,”amesema Hajib.

Hajib ambaye aliondoka Alhamisi iliyopita nchini kwenda Misri kwa majaribio ya kucheza soka ya kulipwa baada ya kupewa baraka zote na uongozi wa Simba.

Source: Bin Zubeiry Sports

 

Share.

About Author