HIVI NDIVYO JUMA NYOSO ALIVYO TAKA KUMPIGA HAJI MANARA - The Choice

HIVI NDIVYO JUMA NYOSO ALIVYO TAKA KUMPIGA HAJI MANARA

0
----mwisho-----

Jana moja kati ya Tukio lililokuwa Gumzo lilikuwa ni lile la Juma Nyosso beki wa kati wa Kagera Sugar kumtwanga Shabiki ambaye inasemekana alimtamkia maneno ya Kumkera mara baada ya Mchezo ulioisha kwa Kagera kufungwa bao 2 kwa 0.

Moja kati ya vitu ambavyo watu wengi hawakujua msomaji wa Kwataunit.com  Juma Nyosso alianza umwamba toka tu mpira Ulipomalizika wakati anatoka uwanjani inadaiwa kuwa Msemaji wa Klabu ya Simba Haji Manara naye alikuwa anaingia uwanjani(Kwenye uzio wa Pitch)

Baada ya Kukutana wawili hao Nyosso alimsukuma Haji Manara na Manara ikabidi tu awe Mpole na Kupitia ukurasa wa Haji Manara wa Instagram Manara ameandika kuhusiana na Tukio Hilo akionekana kusikitika na Kutamba Pia kuwa yeye hajatokea Porini ni mtoto wa Mjini.

” Lau ningekuwa mjinga ningeanza kugombana mm na huyu mchezaji asiyejitambua..kanisukuma bila sababu baada ya game ila nikaona nikichachamaa washabiki wetu wangeweza kumdhuru..uzuri wake niliwaambia Kocha wake Mecky Maxime na nahodha Juma kaseja kabla ya kwenda kumdhuru huyo mshabiki…Nyoso mm sijatoka Buhelelo…Wahangaishe maforeigners mjini….huo undava na uselamavi mm nshavuka huko @official_juma_kaseja#meckymexime “

Bada ya Kumsukuma MANARA na Manara kuamua kukausha tu ndipo baadaye tukio la Kumpiga SHABIKI lilitokea kwahiyo kama Manara angeleta utata  basi ni wazi huenda kichapo kingeanzia kwake.

Share.

About Author