Home Michezo Hizi Ndizo Salamu Za Yanga ” Baada Yakurudisha Jembe lao Kazini

Hizi Ndizo Salamu Za Yanga ” Baada Yakurudisha Jembe lao Kazini

31
0

Ni kama vile faraja inakaribia kurejea ndani ya Klabu ya Yanga baada ya kusikia habari njema kuhusu kiongozi wao wa zamani.

Habari hizo nzuri ni kuwa aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, amekubali kurejea kurejea klabuni hapo endapo baadhi ya viongozi watakubali kuondoka.
Mara baada ya kusambaa kwa taarifa hizo katika mitandao ya kijamii kukachafuka kutokana na Wanayanga wengi kufurahia taarifa hizo

Watu wa ndani wa Yanga wamedai kuwa Manji amekubali kiu ya wanachama na mashabiki wengi wa Yanga waliokuwa wakihitaji uwepo wake, baada ya klabu yao kuyumba kiuchumi wakati akiwa amejiuzulu nafasi ya uenyekiti.Kuelekea mkutano mkuu, jana viongozi wa matawi Yanga walikutana na kujadili mambo kadhaa kuelekea mkutano huo huku wakisisitiza kuwa kauli mbiu itakuwa ni “Yusuf Manji na Mabadiliko”
Mapema jana Bodi ya Wadhamini wa Yanga chini ya George Mkuchika, walikutana na Manji kwa ajili ya kumuomba aweze kurejea wakati klabu ikijiandaa kuelekea mkutano mkuu Juni 10 2018.
Taarifa zinasema baada ya mazungumzo, Manji amewataka baadhi ya viongozi waweze kujizulu kwanza ambao wanaenda kinyume na matakwa yake, kabla hajarejea klabuni hapo huku majina ya watu hao yakiwa hayajatajwa