Huyo Tambwe achaneni naye, - The Choice

Huyo Tambwe achaneni naye,

0

WAKATI straika Mrundi, Amissi Tambwe, akiwa hajacheza mechi hata moja msimu huu kutokana nakuwa majeruhi, rekodi yake tangu ametua nchini inazidi kuwabana wakali wa mabao Ligi Kuu Bara; Emmanuel Okwi wa Simba na Obrey Chirwa wa Yanga.

Kwanza, Tambwe hajawahi kumaliza msimu bila kufunga mabao  11 ama zaidi, jambo ambalo linawabana Chirwa na Okwi kuhakikisha wanaifikia kwa kufunga mabao matano kwa matatu mtawalia. Rekodi ya mabao machache zaidi kwa Tambwe ni msimu uliopita alipofunga mara 11.

Pili, Tambwe ndiye mchezaji wa kizazi kipya aliyewahi kufunga mabao 21 kwenye msimu mmoja, akifanya hivyo msimu uliopita.

Okwi mwenye mabao manane Ligi Kuu atahitaji kufunga mara 13 katika mechi 19 zilizosalia ili kuifikia rekodi hiyo ya Tambwe. Kwa upande wa Chirwa anahitaji mabao 15 katika mechi zilizosalia ili afikie rekodi hiyo ya Tambwe.

Okwi na Chirwa pia hawajawahi kutwaa tuzo ya Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara, wakati Tambwe amewahi kutwaa mara mbili. Kwa maana hiyo watahitaji kupambana vilivyo ili kuandika rekodi hiyo mpya. Tambwe kwa sasa anajifua ili aweze kurejea uwanjani pindi Ligi Kuu itakapoendelea.

748 total views, 2 views today

Facebook Comments
Share.

About Author