HUYU NDO KOCHA MPYA WA SIMBA ANAYEZIBA PENGO LA OMOG - The Choice

HUYU NDO KOCHA MPYA WA SIMBA ANAYEZIBA PENGO LA OMOG

0

Aliyewahi kuwa Kocha wa Simba, Patrick Phiri raia wa Zambia, anatarajiwa kurudi kikosini hapo kuchukua mikoba ya Mcameroon, Joseph Omog.

Phiri aliyewahi kuifundisha Simba vipindi viwili tofauti, anatajwa kuja kuchukua nafasi ya Mcameroon huyo aliyetimuliwa hivi karibuni.

Chanzo cha habari kutoka ndani ya Simba, kimeeleza kuwa mpango huo wa kumrudisha Phiri unaendelea na muda wowote atapewa mkataba.

“Kuna makocha kadhaa wanaweza kuja kuchukua nafasi ya Omog, lakini Phiri ndiye ana nafasi kubwa ya kuchukua nafasi hiyo, hivyo muda wowote kuanzia sasa anaweza kupewa mkataba.”

3,658 total views, 2 views today

Facebook Comments
Share.

About Author