JERRY Muro Aivua Nguo Yanga, Adai Kuna Wanafiki - The Choice

JERRY Muro Aivua Nguo Yanga, Adai Kuna Wanafiki

0

Aliyekuwa msemaji wa klabu ya Yanga, Jerry Muro amesema kuwa ilikufanikiwa katika utendaji ndani ya uongozi wa mabingwa hao wa kihistoria ni lazima kuangalia ni nani anakuletea ushauri.

Muro ameyasema hayo ikiwa ni sikuchache tu zimepita tangu Yanga imtangaze msemaji mpya wa timu hiyo, Dismass Ten aliyochukua nafasi yake.

“Yanga kuna majungu watu wanapenda wafanye vitu vyao, kuna wanafiki ambao watakwambia ufanye hiki ukikifanya unaingia chaka”. Amesema Jerry Muro aliyekuwa msemaji wa klabu hiyo.

Muro ameongeza kwa kusema kuwa “Wapo Yanga SC watu wenye msaada wa kweli, wazuri sana, wenye akili na wenye mapenzi ya kweli kuhakikisha Yanga inakuwa kama TP Mazembe watu wote hao wapo Yanga”

“Unachotakiwa kufanya ni kufungua macho kuangalia ni nani anakuletea ushauri, maana kuna mwingine anakuletea ushauri wakati yeye kashindwa kuongoza nyumba yake kaachana na mkewe ,hajali watoto wake yeye mwenyewe kufua nguo hafui nguo maisha yake yamemshinda”

Mungu anasema unapojipenda nafsi yako wewe mpende na jirani, kaka kama MTU kashindwa kuendesha familia yake kamwe hawezi kuendesha Yanga”. Muro ameyasema hayo kupitia chombo cha habari cha UFM radio.

Share.

About Author