Jinsi rais wa Etoile Du Sahel atakavyoitajirisha Yanga kwa mamilioni - The Choice

Jinsi rais wa Etoile Du Sahel atakavyoitajirisha Yanga kwa mamilioni

0
----mwisho-----

Klabu ya Yanga huenda ikapata mamilioni ya kutosha tu  kutoka Etoile Du Sahel kwani Rais wa Klabu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia Ridha Charfeddine  anadaiwa kumsumbua Meneja wa Mchezaji Yohanna Nkomola Mwinyi Kambi kuhusu Kumwitaji Kinda Huyo zao la Serengeti Boys.

Inadaiwa rais wa Klabu ya Etoile amesema yuko tayari kutoa Kitita Chochote cha pesa ili kumsogeza Yohanna kwenye timu hiyo, Naye Mwinyi Kambi amesema Klabu ya Yanga iko tayari kwa Mazungumzo na Etoile ili kuangalia uwezekano wa Kufanya biashara.

Yanga kama ikifanikiwa kumuuza Nkomola basi huenda ikapata mkwanja wa Kutosha kwani timu za Kiarabu zimekuwa zikitoa Mkwanja mrefu sana zinapomwitaji mchezaji wanayemuona ni mzuri.

Ikikumbukwa kwa Emmanuel Okwi wakati anatoka Simba kwenda kwao aliuzwa zaidi ya dola 300,000 zaidi ya milioni 600 za Kitanzania wakati huo huo Yanga nayo ikiwa imeonja utamu wa Kuuza Wachezaji kwa waarabu kwani walikula zaidi ya Milioni 200 mchezaji Simon Msuva kwenda Al Jadida ya Morocco.

Nkomola  aliwahi kwenda Etoile Du Sahel kwaajili ya Majaribio na Alifaulu majaribio yake na kuwa kwenye timu B ya Etoile lakini walishindwa kukubaliana baadhi ya Vitu hali iliyomfanya Nkomola kurudi nchini na Yanga wakaona Wasimcheleweshe kumpa Kandarasi.

Share.

About Author