Jose Mourinho; Najiskia vibaya kuhusu Depay na Ashley Young. - The Choice

Jose Mourinho; Najiskia vibaya kuhusu Depay na Ashley Young.

0

jm

Manager Jose Mourinho ameweka wazi kuhusu kushindwa kuwapa nafasi vizuri wachezaji wote wa kikosi ambacho anakiongoza. Jose amekili kwamba kuna wachezaji ambao hajawapa nafasi yakuonyesha uwezo wao kwenye kikosi.

Wachezaji hao wengi wao wameshaanza kujitayarisha kujiunga na club nyingine kwa mkopo au kuondoka moja kwa moja. Mmoja ya wachezaji wenyewe ni Depay. Mwingine ambae bado anapambana kupata namba ni Ashley Young. Kutokana na Manchester kujihusisha sana na uwezekano wa kuwaleta wachezaji kama Antoine Griezmann kunaendelea kupunguza uwezekano wa wachezaji hawa kupata nafasi.

Mourinho aliimbia SkySport hivi,“Bado najiskia vibaya juu yangu kwasababu sijampa nafasi kila mmoja kuonyesha kile alichokua nacho. Kwenye nafasi nyingine kwenye kikosi chetu tunawachezaji wengi sana. Kuwa mkweli kwa watu kama Ashley Young na Memphis Depay sijawapa nafasi za kutosha kucheza kuonyesha uwezo wao.”

Kwa upande wa Ashley Young mambo hayapo wazi kama ataondoka United lakini kwa Depay imekuwa wazi sana kwamba atajiunga na Everton ikifika January.

Facebook Comments
Share.

About Author