Home Mahusiano Joyce Kiria anawakilisha wanawake wapumbavu duniani? . Je, Kilewo anatudhalilisha wanaume!?

Joyce Kiria anawakilisha wanawake wapumbavu duniani? . Je, Kilewo anatudhalilisha wanaume!?

354
0

Joyce Kiria anawakilisha wanawake wapumbavu duniani? . Je, Kilewo anatudhalilisha wanaume!?

Ni kweli wanawake wengine ni stubborn si kidogo,. Na wengi ni nature yao. Mwanamke silaha yake kubwa ni “mdomo” narudia “mdomo “. Na ukimkanya kidogo (kwa kibao kidogo) hata cha huba atapiga kelele mithili ya kuku aliye taga kwa mara ya kwanza.

Katika mazingira hayo, wanaume wasio na busara na hekima zawadi pekee anayo weza mpatia mwanamke ni kipigo. Nasema atasema anamfunza adabu.” Kosa”

Maandiko ya Biblia yanaeleza wazi kuwa mwanaume atabaki kuwa Kichwa cha familia ikisaidiana na mkewe kwa karibu. Km Kichwa cha nyumba baba yafaa uelewa tabia za mwanamke, na uishi nae kwa akili. Narudi kwa akili! Tofauti na hapo aibu itakuwa ya kwako hata kama kosa ni lake. Haitakuwa tofauti na unapo kuwa unaoga, halafu atokee kichaa abebe nguo zake, then uenze kumkimbiza. Matokeo yake ama wote mtaonekana viachaa au wanao kujua watajua wew ndiwe umerukwa na akili.

Wanawake wameumbwa na hisia kali “Emotional” ndio maana anaweza kukwambia nipige “uone! Na ukimtazama ni mtu ambaye hampo nae sawa kinguvu na ukimtia “kelb” moja ya kumfundisha adabu ataanza kupiga mayoweeee.. Ukimuacha atasema “una muogopa ” Nini kifanyike, Wanaume ishini na wake zenu kwa akili.

Kuna wanawake wengine ni wagomvi wanawagombeza waume zao popote walipo, wanawatusi, wana wapiga wanaume, tena vipigo vikali si kidogo. Wengine huwa wanawafungia nje, na wakati mwingine huwatimua kabisa, ila maskini wanaume, wao machozi ya Samaki, maumivu ndani kwa ndani “Akisema sana atamwambia mshikaji wake wa karibu!
Na wanaume nanyi tokea, mbona wao mkiwapiga kiduchu, ni kelele mtaa mzima? That’s fair?

Aidha, Wanaume wanao kutana na madhila hao ama ni :-
*wanaume wanao lishwa, na kutunzwa na na wanawake wanao jiweza kiuchumi “mamaz au dadaz” yaani kazi yao = msingi ni kiuno. Ujinga!

*Wanaume wasio timiza majukumu yao ya ndani ya “ndoa ” Sasa hapa Kuna sababu kadhaa ama ni tatizo la kimaumbile, tatizo kiafya, au Uvivu tu. Hapa lazima mwanamke awashe moto ndani. “Ji-adjust”

*Au sababu nyingine ni mwanaume kukosa msimamo, yamkini mwanamke ana uchumi imara kuliko wew, ila ukisha poteza legitimacy ya kimawazo, kifikra na msimamo nyumbani. Usitegemee kuheshimiwa hata na wanaume wenzio uraiani.

Mwsho, siungi mkono udhalilishaji wa kumpiga mwanamke, ila hadi kufikia kiwango cha kumtwanga mwanamke ni ishara kuwa wew mwanaume huna na umekosa ushawishi, Mwanamke amesha jua udhaifu wako, amesha kuvuta katika level zake, hivyo anakufanya anavyo ona inafaa. Ndoa nyingi mno, huwa uwanja wa ugomvi na sababu kubwa ni mwanaume kutosimama katika nafasi yake.

Nini Maoni Yako?