Kifurushi cha hairisha mchezo wa Man Utd - The Choice

Kifurushi cha hairisha mchezo wa Man Utd

0

Mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya Uingereza baina ya Manchester United na Bournemouth umehairishwa kufuatia kubainika kwa kifurushi kinachotiliwa shaka katika dimba la Old Trafford.

Polisi akiwa na Mbwa wa kunusa milipuko katika uwanja wa Old Trafford.
Mashabiki katika majukwaa mawili ya Sir Alex Ferguson na Stretford End, waliondolewa kabla ya kuanza kwa mchezo huo na mbwa wa kunusu milipuko waliletwa ili kusaidia kubaini kifurushi hicho.
Awali nchezo huo ulicheleweshwa kuanza na kisha muda mfupi baadae mechi hiyo ilihairishwa kabisa kufuatia ushauri uliotolewa na polisi. Maafisa usalama walisimamia zoezi la mashabiki kutoka nje ya uwanja

Facebook Comments
Share.

About Author