Home Michezo Kikosi cha Simba Kinachoweza kuanza dhidi ya Prisons Leo 16.4.2018

Kikosi cha Simba Kinachoweza kuanza dhidi ya Prisons Leo 16.4.2018

246
0

Hiki ni Kikosi cha Utabiri cha Simba Kinachoweza kuanza leo dhidi ya Tanzania Prisons mechi ya Ligi Kuu katika uwanja wa Taifa Jijini Dar Es Salaam.

Golini : Aishi Manula anabaki kuwa kipa namba Moja wa Simba kutokana na uwezo wake awapo Langoni.

Mabeki wa pembeni : Nicolas Gyan na Asante Kwasi bila shaka Mwalimu Pierre Lechantre ataendelea kuwaamini kutokana na Performance yao kwenye michezo iliyopita.

 

Mabeki wa Kati na Viungo : Katika Mchezo uliopita Kati ya Simba na Mbeya City Tulishuhudia Simba Ikichezesha wachezaji watatu wenye asili ya mabeki wa KATI yani Yusuph Mlipili, Juuko Murshid na Erasto Nyoni bila shaka   hata Leo ndivyo watakavyoanza

Huku Jonas Mkude  akiwa ndiye namba 6 Asili na Shomari Kapombe akicheza kama Kiungo mwingine lakini akicheza kutokea pembeni kama namba 7 ambaye anacheza zaidi eneo la Kati na Hivyo Kumruhusu Erasto Nyoni kucheza kama namba 8 pia huku wakibadilishana na Shomari Kapombe wanapokuwa uwanjani.

Namba 11 Shiza Kichuya ambaye ndiye Bingwa wa Assist mpaka sasa ataanza kama winga wa kushoto, Na Bocco na Okwi kusimama kama Washambuliaji wa Kati.

Aishi Manula, Nicolas Gyan,Asante Kwasi, Yusuph Mlipili, Juuko Murshid, Erasto nyoni, Jonas Mkude, Shomari Kapombe, John Bocco, Emmanuel Okwi, Shiza Kichuya.