Kikosi cha Simba kinachoweza Kuanza Leo dhidi ya Maji Maji. - The Choice

Kikosi cha Simba kinachoweza Kuanza Leo dhidi ya Maji Maji.

0

Kikosi cha Simba kinachoweza Kuanza dhidi ya Maji Maji Leo

Huu ni Utabiri wa Kikosi cha Simba kinachoweza Kuanza leo katika mchezo wa raundi ya 15 Ligi Kuu soka ya Tanzania BARA VPL 2017/2018

Golini : Bila shaka golini atakuwepo golikipa ambaye amecheza mechi za Nyuma 14 na kuonekana kuaminiwa Aishi Salum Manula.

Mabeki wa Pembeni : Shavu la Kushoto Asante Kwasi hakuna Ubishi kuwa ataanza katika mchezo wa leo. Shavu la Kulia huenda Shomari Kapombe ambaye alionekana kuwafurahisha wanamsimbazi kwenye mchezo kati ya Kagera na Simba mara baada ya Kuingia na Kutoa pasi safi ya Bao

Mabeki wa Kati : Erasto Nyoni na Juuko Murshid MSOMAJI wa Kwataunit  wameonekana kuanza kuelewana katika michezo ya Hivi karibuni na Kutokana na wachezaji waliopo kikosini ni wazi bado wataendelea kuaminiwa msomaji wa Kwataunit hata katika mchezo wa Leo dhidi ya Maji Maji Uwanja wa Taifa.

Viungo wa pembeni : James Kotei ambaye Siku za Karibuni amekuwa akicheza kama namba saba huenda akaendelea kuaminiwa na Mwalimu Pierre Lechantre akisaidiana na Masoud Djuma hii inatokana na kwamba Kotei akicheza pembeni anauwezo wa Kusaidia hata kucheza katikati ya uwanja. Wakati namba 11 Huenda Said Ndemla akacheza kutokana na kiwango kikubwa siku za Karibuni.

Viungo wa Kati : Kama ilivyokuwa katika mChezo Uliopita NAMBA 6 Jonas Mkude na Namba 8 Shiza Kichuya, Najua umeshtuka kumuona Kichuya kama namba 8 Uwepo wa mtu kama Kotei uwanjani na Kapombe upande Mmoja wa Kulia unaweza ukafanya Simba kucheza kama wameua Winga ya Kulia na Kumfanya Kapombe Kusogea mbele zaidi na Kotei kusogea katikati ya uwanja na Hii inamfanya Kichuya kuwa na Uwezo wa Kutokea Popote pale uwanjani.

Washambuliaji : Bila Shaka John Raphael Bocco atasimama kama Mshambuliaji wa Kati akisaidiana na MGANDA Emmanuel Okwi ambaye amekuwa hafanyi sana Vizuri Mkoani lakini Unapomsogeza Taifa muda wowote anafunga.

Huu ni Utabiri tu kikosi chenyewe kitatolewa baadaye na sisi tutakuwekea, Kumbuka Kulike Ukurasa wetu wa Facebook hapo chini.

Share.

About Author