Kocha kafafanua kilichopelekea Mwadui ‘kufa’ kwa Yanga dakika za usiku - The Choice

Kocha kafafanua kilichopelekea Mwadui ‘kufa’ kwa Yanga dakika za usiku

0

Na Zainab Rajab

Baada ya kufungwa na Yanga, kocha msaidizi wa Mwadui FC Khalid Adam amesema, kilicoigharimu timu yake ni makosa ya kiuchezaji ambayo yalifanywa na wachezaji wake.

“Makosa ya kiuchezaji sio suala la kuzidiana, kwenye mchezo wa mpira wa miguu ukifanya kosa moja mwenzako analitumia, tumefanya makosa wenzetu wametumia nafasi,” anasema Halid Adam kocha msaidizi wa Mwadui.

“Makosa ya golikipa yanavyotokea kwenye mchezo ni sehemu ya mchezo kwahiyo kama yanajirudia tunayafanyia kazi tuweze kuyarekebisha.”

Golikipa wa Mwadui FC Shabani Kado amekuwa akikosolewa kwa kufanya makosa yanayojirudia uwanjani ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakisababisha timu yake kupoteza mechi.

Adam amesema walijitahidi kucheza kwa umakini katika kipindi cha kwanza likatokea kosa wakafungwa goli ambalo liliwakatisha tamaa wachezaji wao.

Kocha huyo pia akakiri kuwa, walikutana na Yanga timu ambayo inawachezaji wengi wenye uzoefu, walijitahidi kushindana lakini bahati haikuwa yao hivyo wamekubali matokeo waliyopata kwenye mchezo dhidi ya Yanga.

Share.

About Author