Tazama Hapa Alichosema Ommy Dimpoz Juu ya Mjengo Wake Anaoporomosha Huko Mbezi..!!! - The Choice

Tazama Hapa Alichosema Ommy Dimpoz Juu ya Mjengo Wake Anaoporomosha Huko Mbezi..!!!

0
Msanii wa muziki wa bongo fleva Ommy Dimpoz ambaye bado anafanya vyema na wimbo wake ‘Kajiandae’ amefunguka na kusema hajapangishiwa nyumba Mbezi na jimama kama ambavyo inadaiwa na kudai kuwa kwa sasa yeye anaishi Mikocheni.
Ommy Dimpozi akiongea na EATV alisema hana nyumba ambayo amepangisha wala hajapangishiwa nyumba ila kwa sasa anafanya ujenzi katika viwanja vyake viwili Mbezi pamoja na Kigamboni.
“Unajua binadamu wanaweza kuongea hiki na hiki lakini ukweli ni kwamba mimi naishi Mikocheni kwenye apartment hivyo siishi Mbezi, ila Mbezi kuna sehemu nina site yangu ambayo najenga na site nyingine ipo Kigamboni.
Kwa hiyo sina nyumba ambayo nimepangisha au nimepangishiwa kwa hiyo hizo stori sijui bimkubwa sijui nini siyo kweli, mimi mambo yatakapokuwa tayari nitamuweka wazi mtu wangu ila demu wangu si Mzungu ni Mchina” alisema Ommy Dimpoz.
Facebook Comments
Share.

About Author