Kwa hili Ndemla umekosea ,Muombe msamaha Kocha Masoud Djuma - The Choice

Kwa hili Ndemla umekosea ,Muombe msamaha Kocha Masoud Djuma

0

Katika wachezaji ambao ni wastarabu na wenye nidhamu ya khali ya juu basi huwezi kumuacha Ndemla,Ndemla ni kijana anayependwa sana na washabiki na wapenzi wa Simba.

Kwa nini nasema Ndemla amekosea na anapaswa kumuomba msamaha kocha wake,hii inatokana na kitendo chake cha kutompatia mkono mwalimu pale alipofanyiwa mabadiliko katika kipindi cha kwanza katika mchezo dhidi ya Mbao na nafasi yake kuchukuliwa na Mdhamiru Yassin.

Kitendo kile dhahiri Ndemala hakukifurahia ndo maana alikataa hata kumpatia kocha Masoud mkono.Kitendo ambacho sio nidhamu nzuri aliyo ionyesha mbele ya mwalimu na anapaswa kumuomba msamaha mwalimu wake.

Share.

About Author