Man City kuivaa Real Madrid-UEFA. - The Choice

Man City kuivaa Real Madrid-UEFA.

0

Michuano ya klabu bingwa barani Ulaya hatua ya Nusu fainali inaendelea tena leo ambapo Manchester City watamenyana na Real Madrid.

Manchester City wataikaribisha Real Madrid katika Mechi hiyo huku wakiwa na pigo kubwa la kumkosa Kiungo wao kutoka Ivory Coast, Yaya Toure.

Katika mchezo mwingine Atletico Madrid na Bayern Munchen watakukutana kesho jumatano Jijini Madrid katika Mechi ya Kwanza ya Nusu ya klabu bingwa barani ulaya uwanja wa Estadio Vicente Calderon

Atletico chini ya Kocha Diego Simeone wanatinga hatua ya Nusu Fainali kwa mara ya pili ndani ya Miaka Mitatu wakati Bayern, ambao sasa wapo chini ya Kocha Pep Guardiola, hii itakuwa ni Nusu Fainali yao ya tano mfululizo, Fainali ya Michuano ya hii itapigwa jumamosi tarehe 28 .

Share.

About Author