Maskini Gabriel Jesus. - The Choice

Maskini Gabriel Jesus.

0
----mwisho-----

Gabriel Jesus limeshaanza kuwa jina linalotajwa sana miongoni mwa mashabiki wa soka.Usajili wa £27m kutoka Palmeiras kwenda Man City umemfanya umaarufu wake uweze kuongezeka.Katika mechi mbili zake na City katika ligi kuu ya Uingereza amefanikiwa kufunga goli 3 hali iliyomlazimu kocha Pep Gurdiola kumuanzisha yeye huku mshambuliaji hatari Kun Aguero akianzia benchi.Tayari nyota wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Brazil Ronaldinho Gaucho amemtabiria Jesus kuwa Messi ajae.

Ndoto za Jesus kufanya makubwa zaidi msimu hu zinaweza kuwa mashakani au kupotea kabisa.Katika mchezo wa Man City dhidi ya Fc Bournamouth Jesus alitolewa uwanjani dakika ya 13 baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Kun Aguero.Majeraha ya Jesus hayakuonekana makubwa sana kwani baada ya kutoka alionekana nyuma ya jukwaa la City halu iliyoashiria hakuwa katika hali mbaya sana.
Lakini si hivyo,Jesus ameumia.Jesus ameumia kwani sasa hawezi kutembea vizuru na amekuwa akitumia magongo maalumu.Ripoti za madaktari zinasema Jesus anaweza kukaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu.Huu ni mwezi wa pili na kukaa nje miezi mitatu ni kwamba Jesus itabidi asubiri hadi mwezi wa tano ndio arudi uwanjani.Mwezi wa tano ndio mwisho wa msimu kwahiyo Jesus atakuwa nje kwa muda wote wa msimu uliobaki.
Ni pigo kubwa kwa Pep Gurdiola kwani alikuwa akimtegemea sana Jesus na baada ya mechi dhidi ya Fc Bournamouth Gurdiola alisema “siwezi sema kitu chochote kuhusu Jesus kwa sasa na usiku huu inabidi tumuombe mungu isiwe jambo kubwa sana arudi uwanjani haraka” lakini sasa ombi la Gurdiola linaonekana kukwama kwani Jesus hatakuwepo tena uwanjani jadi mwezi wa tano.
Hii inaweza kuwa habari njema kwa mshambuluaji Kun Aguero.Aguero tangu kuwasili kwa Jesus nafasi yake uwanjani imekuwa finyu sana.Alishuhudiwa akiingia uwanjani dhidi ya Fc Bournamouth baada ya Jesus kuumia.Kuumia kwa Jesus kunamaanisha Pep Gurdiola itamlazimu kumtumia Kun Aguero.
Share.

About Author