Mcheza Mpira Okwi Ajitapa Kufunga Goli Moja Katika Mchezo wa Kesho - The Choice

Mcheza Mpira Okwi Ajitapa Kufunga Goli Moja Katika Mchezo wa Kesho

0
Okwi Ajitapa Kufunga Gori Moja  Katika  Mchezo wa Kesho

Mshambuliaji wa kimataifa wa Simba, raia wa Uganda, Emmanuel Okwi amefunguka kwa kujitapa kuwa kuelekea mechi dhidi ya watani wa jadi Yanga ‘Ngao ya Hisani’ kesho (Jumatano) atahakikisha anaifunga Yanga japo amepatwa na kitete kusema ni magoli mangap

Okwi ameeleza hayo kupitia mahojiano maalum aliyofanya na klabu yake na kusema hawezi kusema ni magoli mangapi atawapachika ‘gongo wazi’ Yanga kwa kuwa ni klabu ambayo anaiheshimu.
“Game ya Yanga siku zote haiwagi rahisi kwa upande wowote kwa kuwa ni timu yenye wachezaji wazoefu wengi japo na sisi tunawachezaji wazoefu wengi kama wao, tunategemea mchezo wa kesho utakuwa mzuri pia tunamatumaini tutashinda”, alisema Okwi.

Pamoja na hayo, Okwi aliendelea kwa kusema “nitahakikisha timu yangu inashirikiana vizuri na wachezaji wenzangu ili tuweze kutoka na matokeo mazuri katika mchezo huo. Siwezi kusema tutawafunga magoli mangapi kwa kuwa ni timu ambayo ninaiheshimu lakini sisi tutajipanga kuhakikisha tunatoka na matokeo mazuri”, alisisitiza Okwi.

Okwi ameanza tambwe hizo ikiwa imebakia siku moja kuchezwa kwa mechi ya watani wa jadi siku ya kesho (Jumatano) ambapo mchezo huo umekuwa ukisubiliwa na watu mbalimbali waweze kujua ni nani siku hiyo ataweza kumfunika mwenzake.

Share.

About Author