Mourinho ampa Martial mtihani wa mwisho. - The Choice

Mourinho ampa Martial mtihani wa mwisho.

0
----mwisho-----

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na hali ya sintofahamu kati ya Jose Mourinho na mchezaji wake Anthony Martial.Inasemekana wawili hao hawaivi siku hizi na tetesi zinasema Jumatatu iliyopita Martial hakuhudhuria Carrington kufanya mazoezi na timu.Mourinho sio tu kwamba ana tofauti na Martial ila inasemekana watu wote walio karibu na mchezaji huyo hawako katika uhusiano mzuri ma Mourinho.

Inaaminika kwamba Mourinho alikerwa na kiwango cha Martial katika mechi dhidi ya Liverpol.Martial alicheza upande ambao Liverpool walimuweka kinda wa miaka 18 Alexendre Arnold lakini Martial hakuonesha lolote mbele ya dogo huyo.Mourinho alimtoa Martial na mechi iliyofuata dhidi ya Stoke City hakuwepo hata benchi vivyo hivyo mechi dhidi ya Hull City hali inayoonekana kumchukiza Martial.
Hii sio mara ya kwamza kwa Mourinho kutofautiana na Martial.Mwishoni mwa mwaka jana Mou alimrushia dongo wakala wa mchezaji huyo Phillipe Lamboley.Mourinho anaamini Lamboley anamdanganya Martial na kumfanya asitulie.Mourinho alimuambia Martial aache kuwasikiliza watu wengine bali amsikilize yeye tu kama kocha.
Sasa baada ya yote haya Mourinho kaja na mpya juu ya Martial.Mourinho ni kama anamtega Martial au anatumia njia hii kumfanya ajitume.Manchester United wana mchezo wa FA dhidi ya Wigani na kocha Josee Mourinho mechi hii ameamua kuitumia kama mtihani kwa Martial.
Akiongea na waandishi wa habari alisema “sijui anavyojisikia nikimuacha nje kwa kuwa siulizagi wachezaji kuhusu hilo,lakini Jumapili atacheza na kama akicheza vizuri nitampa nafasi katika mechi ijayo ya lihi dhidi ya Hull City”.Hii ina maana kama Martial akiboronga atakuwa kwenye wakati mgumu tena katika ligi kuu.
Martial ameanza kuwa kipemzi cha mashabiki wa United.Lakini sio mara ya kwanza kwa Jose Mourinho kugombana na wachezaji wanaopendwa sana na mashabiki wa timu.Kama inakumbuka alimuuza Juan Mata kwenda United kipindi ambacho alikuwa akipendwa Chelsea.Uhusiano wa Mou na Martial umekuwa mbovu kiasi kwamba tayari ameshaanza na kuhusishwa na kuondoka Man United.
Share.

About Author