MPYA HII: MANCHESTER UNITED YAMNASA ROMELU LUKAKU, ROONEY KUTIMKIA EVERTON - The Choice

MPYA HII: MANCHESTER UNITED YAMNASA ROMELU LUKAKU, ROONEY KUTIMKIA EVERTON

0

Manchester United are set to announce the signing of Romelu Lukaku for a £75million fee
Habari zinazoendelea kushika kasi katika mitandao mbali mbali duniani hivi sasa ni Klabu ya Manchester United kufanikiwa kuingia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku.

United imemgeukia Lukaku baada  ya dili la kumsajili mshambuliaji Alvaro Morata wa Real Madrid kukwama ikionekana kabisa Real Madrid hawako tayari kumuuza mshambuliaji huyo.

Paundi milioni 75 zimetajwa kuwa ndiyo ada itakayolipwa na manchester United huku utambulisho ukitarajiwa kuwa leo Alhamisi japokuwa hakuna taarifa yoyote rasmi kutoka katika klabu hizo mbili wala kwa mchezaji mwenyewe mpaka sasa.

Wakati huo huo Wayne Rooney ambaye ni nahodha wa Manchester United anatarajiwa kuihama klabu hiyo na kurejea Everton ambako ndiko hasa alikoanzia maisha ya soka kwa uhamisho ambao haujatajwa kama unaendana na huu wa Lukaku.

Share.

About Author