Msimu huu ndiyo mwisho kwa Simba kufanya vibaya - The Choice

Msimu huu ndiyo mwisho kwa Simba kufanya vibaya

0

Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva.

Aliongeza kuwa wamepanga kutumia kasi kikubwa cha fedha kipindi hiki kusajili wachezaji wenye uzoefu mkubwa kwa ajili ya kubeba ubingwa wa Tanzania na hata kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa.

“Tumekubaliana na viongozi wenzangu kubadili mfumo wetu wa kusajili sasa kuanzia msimu ujao tunataka kuwa na kikosi madhubuti ambacho kitatupa ubingwa wa Vodacom lakini pia kufanya vizuri kwenye mashindano yote tutakayoshiriki na tayari tumeshatenga fedha za usajili kuhakikisha hilo linatimia,” amesema Aveva.

Kiongozi huyo amesema wamechoka kuchekwa na wapinzani wao Yanga ambao kwa sasa wamekuwa kwenye mafanikio makubwa kwa kutetea taji lao la Vodacom lakini pia wamefika fainali ya Kombe la FA watakayocheza na Azam na pia wapo katika nafasi nzuri ya kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF).

Facebook Comments
Share.

About Author