Mtoto wa Zidane amefunga goli kwenye mechi yake ya kwanza Real Madrid - The Choice

Mtoto wa Zidane amefunga goli kwenye mechi yake ya kwanza Real Madrid

0
Kocha wa Real Madri Zinedine Zidane akimpa maelekezo mtoto wake Enzo kabla hajaingia uwanjani
Kocha wa Real Madri Zinedine Zidane akimpa maelekezo mtoto wake Enzo kabla hajaingia uwanjani

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema ilikuwa ni ‘special’ kwa mtoto wake Enzo kufunga goli kwenye mchezo wake wa kwana siku ya Jumatano kwenye mechi ya Copa del Rey hatua ya 32 bora mchezo wa marudiano uliomalizika kwa Madrid kushinda kwa magoli 6-1 dhidi ya La Cultural na kufuzu hatua inayofuata kwa jumla ya magoli 13-2.

Mechi ya kwanza ilimalizika kwa Madrid kushinda magoli 7-1, ushindi wa mechi ya marudiano ulichangiwa na Mariano Diaz aliyefunga hat-trick huku James Rodriguez naye akiingia kwenye orodha ya wafungaji.

Enzo Zidane aliingia kutoka benchi na kufunga goli kwenye mchezo wake wa kwanza katika klabu ya Real Madrid wakati ikicheza dhidi ya Cultural Leonesa
Enzo Zidane aliingia kutoka benchi na kufunga goli kwenye mchezo wake wa kwanza katika klabu ya Real Madrid wakati ikicheza dhidi ya Cultural Leonesa

Yeray Gonzalez aliifungia La Cultural bao la kufutia machozi wakati Cesar Morgado akiongeza idadi ya magoli kwa Madrid kutokana na goli lake la kujifunga dakika za lala salama.

Kipindi cha pili Zidane alimpa nafasi mtoto wake Enzo, kinda huyo mwenye miaka 21 alifanya atttempt dakika tano baada ya kuingia kwenye mchezo huo uliokuwa ni wa kwanza wa mashindano kwake kwenye timu ya wakubwa kabla ya kufunga bao akiwa umbali wa mita 20.

Mtoto wa Zidane alifunga goli la nne katika ushindi wa magoli 6-1 walioupata Real Madrid
Mtoto wa Zidane alifunga goli la nne katika ushindi wa magoli 6-1 walioupata Real Madrid

Baada ya mechi, kocha huyo wa The Blancos  aliwaambia waandishi kuwa alifurahishwa na kijana wake lakini pia na vijana wengine kama Martin Odegaard, Alvaro Tejero na Ruben Yanez.

“Nikivua majukumu yangu ya ukocha, nimefurahishwa sana na mwangu,” alisema Zidane. Lakini nikiwa kama kocha wake nimefurahishwa pia na Odegaard, Alvaro pamoja na Ruben na wachezaji wote waliofanya kazi nzuri. Nikifika nyumbani tutazungumza kuhusu hilo.

Wachezaji wengi waliozoeleka kuonekana uwanjani kama Cristiano Ronaldo, Sergio Ramos na Luka Modricwalipumzishwa kuelekea mchezo wa Jumamosi dhidi ya Barcelona huku kiungo Casemiro akirejea kwa mara ya kwanza tangu alipovunjika mguu mwezi Septemba kwenye mchezo dhidi ya Espanyol.

Facebook Comments
Share.

About Author