NI WAKATI WA CHIRWA KUKATAZWA KUPIGA PENATI TENA - The Choice

NI WAKATI WA CHIRWA KUKATAZWA KUPIGA PENATI TENA

0

 

Kwa rekodi Hizi Chirwa siyo Mpiga Penati Mzuri

Endapo jana Yanga ingemaliza Mchezo bila Ushindi ni wazi lawama nyingi zingerudi kwa Mchezaji Obrey Chirwa ambaye alikosa penati baada ya Mchezaji Hassan Kessy kuangushwa kwenye eneo la Penati (Penalty Box) na kuamliwa Kuwa tuta.

Ya Chirwa Kukosa penati hayakuishia uwanjani kwani kwenye mitandao ya Kijamii washabiki wengi walionekana wazi kuchukizwa na tabia ya benchi la Ufundi kuendelea kumwamini Chirwa kwenye suala la Upigaji penati.

Inawezekana ni mchezaji anayepiga vizuri penati awapo mazoezini lakini amekuwa akishindwa kufanya hivyo uwanjani na rekodi zitakozofuata chini zitakuonyesha wazi kuwa nachokiandika namaanisha.

Kwanza Chirwa Msomaji wa Kwataunit.com amekuwa anapiga penati karibu zote kuelekea Upande Mmoja wa Kulia kwake kwa siku za Karibuni hali ambayo inanifanya nimuone kuwa si mtaalamu sana wa Upigaji wa penati na kwa makipa wanaomfatilia ni rahisi kujua anapaswa kuruka wapi ili kudaka penati zake.

KATIKA PENATI 5 ZILIZOPITA KAPATA MBILI TU.

Rekodi huwa hazidanganyi katika penati zake 5 zilizopita Obrey Chirwa amefunga penati mbili tu na Kukosa 3, Hapo Kuna Mpiga penati Kweli? Angekuwa amekosa atleast Moja tungesema ni bahati mbaya.

Ila unapokosa nyingi kuliko unazopata kwangu naona unabahatisha bahatisha.

10.1.2018 Obrey Chirwa alikosa penati Nusu fainali ya Mapinduzi Yanga ikicheza na URA.

30.1.2018 Obrey Chirwa alipata penati ya uwanjani Yanga ikicheza na Ihefu na kuja kukosa wakati wa Changamoto ya Mikwaju ya penati ikiwa ni penati yake ya Pili kukosa katika hizi tano za Mwisho kupiga.

6.2.2018 Yanga ikicheza na Njombe Mji katika mchezo wa Ligi Kuu VPL msomaji wa Kwataunit.com Obrey Chirwa alipata penati.

10.2.2018 Yanga ikicheza dhidi ya St. Louis Obrey Chirwa amekosa Penati tena Penati.

Nafikiri Ukibisha kuhusiana na Hili la Chirwa kuonekana wazi si mpigaji mzuri sana wa mikwaju ya Penati basi wewe Njoo na Facts zako tu maana wazungu wanamsemo wao Mmoja wanasema ” No Data no Right to Speak ” Yani ” Ukiwa Hauna data basi hauna haki YA Kuongea “

2,614 total views, 2 views today

Facebook Comments
Share.

About Author