Home Mahusiano Njia 8 za kujiweka ili mwanaume apate nafasi rahisi ya kukuchumbia.

Njia 8 za kujiweka ili mwanaume apate nafasi rahisi ya kukuchumbia.

413
0

Ujanja wa kumfanya mwanaume aweze kukuakuaproach

1. Jiweke nadhifu

Hii ni muhimu katika yote kama wataka mwanaume akutambue. Kitu cha kwanza anachokiangalia mwanaume huwa ni mwonekano wa mwanamke. Mwanaume anapoingia katika chumba, inamchukua sekunde ndogo zana kuamua iwapo anataka kuapproach mwanamke flani au la.

Kama umevalia vizuri na unapendeza, itarahisisha kazi yako sana.

2. Usionekane kama una shughuli

Usijishughlishe sana na simu yako, ama kitabu chako, ama kitu kingine. Unaweza kuwa umeboeka na unajaribu kujiweka buzy, lakini fursa iweza kuwa hivi, kufanya hivyo kunaweza kumfanya mwanaume anayetaka kukuapproach kuona ya kuwa uko buzy sana kiasi cha kuwa atashindwa kukufuata kwanu unaweza usiwe interested na maongezi yake.

3. Je mko level sawa? 

Hii inakinzana na hatua ya kwanza, lakini inaweza kuwa na tatizo iwapo unaoneka kama uko ligi tofauti na mwanaume. Kama utaoneka amakujiweka mtu wa hadhi ya juu wanawake watapenda kukuangalia lakini hawatakuaproach.

4. Mpatie nafasi aongee na wewe

Hata kama uko katika group na marafiki zako halafu mwanaume akakugundua, mwonyeshe interest kwa kumuangalia kwa madakika. Ukiona kama yuko tayari kuongea na wewe, unaweza kujitenga na marafiki zako kwa muda. Aidha unaweza kuanza kuzunguka hio sehemu kiasi ama unaweza kujipeleka mahali ambapo itakuwa rahisi kwa mwanaume huyu kuzungumza na wewe.

5. Usiwe mjeuri

Kama wewe ni mjeuri kwa yeyote, aidha weita ama mmoja wa rafiki yako, inaweza kutokea kuwa mwanaume ambaye anapania kukuapproach kusimamisha ari yake. Hakuna mtu anapenda mtu mjeuri, na hakuna mwanaume angependa kuapproach mwanamke ambaye anaweza kumpuuzia ama kumkataa.

6. Usilazimishe

Utakuwa unajiaibisha iwapo unalazimisha mambo. Wanaume si mabubwi, hivyo ukiwaangalia mara moja na nyingine ama kuwatabasamia, wanajua kuwa uko tayari kuapprochiwa.

7. Usiboe

Kuwa mwanamke mwenye furaha na mwenye hisia chanya mahali popote pale utakapokua. Mwanamke mwenye shangwe huvutia mwanaume yeyote yule. Kama utaonyesha chembechembe za kuboeka, mwanaume anayetaka kukuapproach anaweza kuwa na maswali mengi ya kujiuliza kwani ataona ya kuwa maisha yako huboesha na yasiyo na mwanga.

8. Tabasamu

Onekana jamili, na nafasi ya wewe kufuatwa na wanaume itaongezeka mara dufu. Kupendwa kwa mwonekano wa kwanza ni kama baraka kwa mwanamke yeyote yule ambaye anataka macho ya mwanaume yamwone.