PAUL POGBA AREJEA MANCHESTER UNITED ASAINI MKATABA WA NGUVU - The Choice

PAUL POGBA AREJEA MANCHESTER UNITED ASAINI MKATABA WA NGUVU

0

Paul Pogba akipozi akiwa na jezi ya Manchester United usiku wa kuamkia leo baada ya kukamilisha usajili wakeManchester United rasmi wamekamilisha usajili wa Paul Pobga kwa dau la paundi milioni 100 ambalo limevunja rekodi ya Dunia.Kiungo huyo wa Ufaransa sasa ndiye mchezaji mwenye thamani zaidi Duniani. Pogba amerejea Manchester United ambako aliondoka mwaka 2012 na sasa anarudi klabuni hapo akitokea Juventus ya Italia.Pogba, 23, anatarajiwa kuvaa jezi namba 6 na amesaini mkataba wa miaka mitano unaompatia mshahara wa paundi laki mbili na Elfu tisini kwa wiki.Hata hivyo kuna kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.
Pogba amerejea: Kwanini United wameamua kutangaza usiku wa manane? Hii kidogo inashtua. Lakini sahau kuhusu hilo, Jose Mourinho alisema huu unaweza kuwa usajili wake wa mwisho majira haya ya kiangazi.
Kwahiyo ni ishu gani nyingine itaizunguka Man United?: Juan Mata anaondoka? Bastian Schweinsteiger ataweza kukikwepa kikosi cha akiba? Je, Marcos Rojo atasalimika katika wiki tatu zilizosalia?
Tutaona, lakini sasa jionee kurejea kwa Pogba.
Facebook Comments
Share.

About Author