Pesa nyingi za wachina zimefuta ndoto za star wa Nigeria. - The Choice

Pesa nyingi za wachina zimefuta ndoto za star wa Nigeria.

0

Mnigeria Odion Ighalo ni kati ya wachezaji wa Kiafrika walioko Ulaya ambao walitabiriwa kufanya makubwa zaidi siku za baadae.Kiwango chake na uwezo wake wa ufungaji katika timu yake ya zamani ya Watford vilimfanya aonekane bora hasa katika ligi ngumu kama Uingereza.

Lakini Ighalo ameenda China!Mwenyewe ameonekana kukerwa na usajili wake wa kwenda nchini China.Ighalo anasema kama ni kwenda China angeshaenda siku nyingi lakini alitamani kucheza soka la ushindani kwa sasa na hakuwa tayari kwenda China alitamani kubaki Ulaya kuonesha ubora wake.
Ighalo anasema kama ni kuuzwa ni bora hata angeuzwa West Bromich au Crystal Palace ambao walionesha nia ya kumtaka.“Mpira ni biashara na ni pesa nilitamani kubaki Uingereza na West Bromich Albion na Crystal Palace walinitaka ila kwa kuwa timu inataka faida zaidi walipokuja Wachina walikuwa na kiasi ambacho Watford walikitaka” alisema Ighalo.
Changchun Yatai ya nchini nchini ndio timu iliyofanikiwa kupata saini ya Ighalo kwa mshahara wa £ 190,000 kwa wiki.Kinachomuumiza zaidi Ighalo ni kuhusu familia yake “familia yangu iko hapa (Uingereza),watoto wangu bado ni wadogo na wanasoma pia marafiki zao wako hapa ni ngumu sana kuanza kuwahamisha na kwenda nao China lakini sina jinsi na maisha yanaendelea” aliongeza Ighalo.
Ighalo anaamini kiasi kikubwa cha pesa zilizoletwa na Wachina ndio zimekatisha ndoto zake kubaki Uingereza.Anaamini umri wake wa miaka 27 anapaswa kucheza kila wikiendi na katika ligi yenye ushindani kama ligi kuu ya Uingereza.
Share.

About Author