Home Michezo Rasmi Simba : Habari Mpya Iliyotufikia Asubuhi Hii Kutoka kwenye Kikosi Cha...

Rasmi Simba : Habari Mpya Iliyotufikia Asubuhi Hii Kutoka kwenye Kikosi Cha Simba Leo JumApili

33
0

Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba chini ya Kaimu Kocha Mkuu Masudi Djuma leo wamefanya mazoezi ya mwisho huko Nakuru kujiandaa na mchezo wa fainali michuano ya SportPesa Super Cup dhidi ya Gor Mahia kesho.

Kesho Simba itakuwa na nafasi ya kuandika historia kwenye ukanda wa Afrika Mashariki kwa kuwa timu ya kwanza kucheza katika ardhi ya Uingereza ndani ya dimba la Goodison Park.

Djuma, anayeaminiwa sana na mashabiki wa Simba, sambamba na kikosi chake wameahidi kupambana kuhakikisha wanatwaa taji la SportPesa Super Cup kwa kuwafunga mabingwa watetezi, Gor Mahia.
Akizungumza na waandishi wa habari leo kuelekea mchezo huo, Djuma amesema wamejipanga na watahakikisha wanashinda mchezo huo kwa kuwa kila mmoja anatamani kwenda Uingereza.
“Mimi na wachezaji wangu hakuna aliyewahi kufika, tunataka kwenda England,” amesema

Naye Mkuu wa Idara ya Habari ya klabu ya Simba, Haji Manara amesema wana imani kubwa kwa kocha Djuma na kikosi chake.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Manara amewapa ujumbe maalum kocha Djuma pamoja na wachezaji wa Simba.
“Kocha Masudi Djuma wanasimba wana imani kubwa na wewe. wanajua unao uwezo wa kuongoza kikosi kesho kwa kushinda na timu kucheza soka bora.
“Mohammed Hussein najua unajua thamani ya jezi ya Simba huku ukiwa na kitambaa cha unahodha, nendeni mkapigane kesho kwa manufaa ya nchi, klabu na maisha yenu.
“Mna dakika tisini za kutengeneza historia kubwa ambayo haitasahaulika. Mtakuwa klabu ya kwanza EA kucheza Goodison Park.”Tunawaamini na Tanzania inawategemea…God bless us