Rekodi za Jose Mourinho dhidi ya Pep Guardiola zinzonyesha Man u atafungwa - The Choice

Rekodi za Jose Mourinho dhidi ya Pep Guardiola zinzonyesha Man u atafungwa

0

Jose Mourinho na Pep Guardiola wote ni makocha wa klabu za Uingereza, huku wakifundisha timu zinazotoka katika jiji moja yaani jiji la Manchester, Wakati Mourinho akiwa katika jiji la Manchester, akiifundisha klabu ya Manchester United kwa upande wa Pep Guardiola yeye ametulia zake na Manchester City akiwanoa vijana wa Shekh Mounsour.

Wanaume hawa (Mourinho na Guardiola) ni wapinzani wa muda mrefu na uwepo wao katika jiji moja kunazidi kuimarisha upinzani huo.

Wapi Upinzani wao ulianzia?

Mourinho alifika Camp Nou katika klabu ya Barcelona mwaka 1996 akiwa kocha msaidizi wa Bobby Robson ambapo alikutana kwa mara ya  kwanza na Josep Pep Guardiola, wakati huo (Pep) alikuwa mchezaji wa klabu hiyo akicheza katika nafasi ya kiungo.

Wareno hao(Bobby Robson na Mourinho) waliifundisha Barcelona mpaka pale ambapo Robson aliondoka na nafasi yake kuchukuliwa na muholanzi Louis Van Gaal.

Wote Mourinho na Guardiola walijifunza kutoka kwa Van Gaal, mbinu mbalimbali za kufundisha soka zuri, ingawa, Mhispania (Guardiola) alikuwa bado mchezaji.  Mwaka 2000 Jose Mourinho alitimka zake Barcelona na kuelekea katika klabu ya Benifica ya Ureno

Katika ukocha , (Mourinho na Guardiola) walikutana kama mameneja (makocha) mwaka 2010 wakati Mourinho akiwa na Inter-Millan na kufanikiwa kuifunga Barcelona ya Pep Guardiola  magoli  3-1 katika nusu fainali ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya UEFA.

Katika msimu wa mwaka huo huo, Mourinho alijiunga na wapinzani wa Barcelona, klabu ya Real Madrid, ambapo Mourinho ‘Special One’ ilipigwa goli 5-0 katika mchezo wake wa kwanza wa El Clásico mwaka 2010. Hakika hii hatoisahau.

Upinzani wa makocha hawa haujawahi kuisha, na sasa wanauendeleza katika ligi kuu ya Uingereza Epl huku tayari wakiwa wamekutana katika ligi hiyo mara tatu na Pep Guardiola kufanikiwa kushinda michezo 2 na huku sare ikiwa mchezo mmoja.

Makombe kwa Jose Mourinho.

FC Porto:

Primeira Liga: 2

Taça de Portugal: 1

Supertaça Cândido de Oliveira: 1

UEFA Champions League: 1

UEFA Cup: 1

 Chelsea:

Premier League: 3

FA Cup: 1

Football League Cup: 3

FA Community Shield: 1

Inter-Millan

Serie A: 2

Coppa Italia: 1

Supercoppa Italiana: 1

UEFA Champions League: 1

Real Madrid

La Liga: 1

Copa del Rey: 1

Spanish Super Cup: 1

Manchester United

FA Community Shield: 1

EFL Cup: 1

UEFA Europa League: 1

Vikombe kwa upande wa Pep Guardiola

Barcelona B:

Tercera División: 1

Barcelona:

La Liga: 3

Copa del Rey: 2

Spanish Super Cup: 3

UEFA Super Cup: 2

FIFA Club World Cup: 2

UEFA Champions League: 2

Bayern Munich:

Bundesliga: 3

DFB-Pokal: 2

UEFA Super Cup: 1

FIFA Club World Cup: 1

Jumla ya michezo waliocheza mpaka sasa:

Mourinho: Amecheza michezo 852, ameshinda 562, sare 175 amefungwa michezo 121.

Pep Guardiola: Amecheza jumla ya michezo 530, ameshinda michezo 382, sare 92 amefungwa michezo 56.

Share.

About Author