Rooney kaweka rekodi mpya ndani ya Manchester United - The Choice

Rooney kaweka rekodi mpya ndani ya Manchester United

0

rooney-rekodi

Wayne Rooney ameweka rekodi ya kufunga magoli mengi ndani ya Manchester United kwenye michuano ya Ulaya wakati wakitoa kichapo cha magoli 4-0 mbele ya Feyenoord na kuendelea kuweka matumaini ya kusonga mbele kwenye michuano ya Europa League.

Nahodha huyo wa mashetani wekundu alifunga bao lake la 39 kwenye michuano ya Ulaya ndani ya klabu yake wakati akiunganisha pasi ya Zlatan Ibrahimovic  na kuwaacha wachezaji wa Feyenoord wakilaumu kuwa mfungaji alikuwa kwenye eneo la offside.

rooney-rekodi

Rooney akatengeneza bao la pili ambalo lilifungwa na Juan Mata.

rooney-rekodi-1

Baadaye golikipa wa zamani wa Liverpool alijifunga wakati akiwa katika harakati za kuokoa krosi ya Ibrahimovic kabla ya Jesse Lingard kufunga biashara dakika majeruhi na kumpa Jose Mourinho ushindi mkubwa akiwa kama bosi wa United.

Sare au ushindi wa ugenini dhidi ya Zorya Luhansk kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi A siku ya Alhamisi Disemba 8, itaifanya United kufuzu hadi hatua ya 32 bora.

united-msimamo

  • Kipigo hiki ndio kikubwa kwa Feyenoord kwenye Uefa Cup/Europa League. Walipoteza 5-1 dhidi ya Borussia Monchengladbach mwaka 1986.
  • Juan Mata amefunga mfululizo kwenye mechi za United kwa mara ya kwanza tangu Septemba 2015.
  • United walipiga mashuti 12 yaliyolenga goli (shots on target) dhidi ya Feyenoord, mashuti yao mengi zaidi ndani ya mchezo mmoja kwenye michuano yote msimu huu.
  • Feyenoord, wameshinda mechi moja tu kati ya mechi zao saba zilizopita walizocheza England kwenye michuano ya Ulaya (D2 L4).
  • United hawajapoteza mechi 14 za mashindano ya Ulaya kwenye uwanja wa Old Trafford (pamoja na mechi za kufuzu), wameshinda mechi zote tatu za hatua ya makundi msimu huu
Facebook Comments
Share.

About Author