Samatta Aendelea kung'ala Ubelgiji - The Choice

Samatta Aendelea kung’ala Ubelgiji

0


Mbwana Samatta ameendelea kufanya kweli kwenye ligi ya Ubelgiji baada ya kuifungia tena timu ya KRC Genk wakati ikichomoka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Kortrijk kwenye mchezo wa ligi.

Ni goli la pili mfululizo baada ya siku chache zilizopita Samatta kuifungia timu yake bao pekee lililoipa pointi tatu za ugenini wakati ikicheza dhidi ya AS Eupen.

Samatta alifunga goli lake dakika ya 42 akiunganisha kwa kichwa krosi ya Schrijvers na kuandika bao la pili.

Magoli mengine ya Genk yamefungwa na Siebe Schrijvers dakika ya 38 na Alejandro Pozuelo dakika ya 68 na kuipa Genk ushindi wa magoli 3-0.

Genk ipo nafasi ya nane (8) kwenye msimamo wa ligi yenye timu 16 ikiwa na pointi 34 baada ya kucheza mechi 22. Imeshinda michezo 10, sare nne na kupoteza michezo nane.

Facebook Comments
Share.

About Author