Shilole Adaiwa Kuivuruga ndoa ya Nuh Mziwanda na Nawal - The Choice

Shilole Adaiwa Kuivuruga ndoa ya Nuh Mziwanda na Nawal

0

Stori ambayo ilikuwa inasambaa sana na kuchukua headlines kwenye mitandao ni kuhusu Mwimbaji Shilole kudaiwa kuivuruga ndoa ya Nuh Mziwanda na Nawal ambao kwa sasa wameachana…sasa Soudy Brown kawagonganisha.

Kupitia The Weekend Chat Show ya Clouds TV aliwagonganisha Shilole na Nawal ambao wanadaiwa kutoelewana ambapo kwenye mzungumzo hayo Shilole alipigiwa simu na kuambiwa yupo live kwenye kipindi ambacho Nawal alikwepo.

“Mimi sina tatizo, mlikuwa mnasemaje? Mimi Shishi baby namjua bwana wake kuliko anavyomjua huyo bwana wake anayesema amemuacha mimi namjua kuliko anavyojua. Kwa hiyo anavyosema nimekimbia kichambo nimekimbia kitu gani yeye ndio amekimbia ndoa mapenzi ya watoto utayajua tu ngoma ya watoto haikeshi bwana wee. – Shilole

Share.

About Author