Sifa 12 kuweza kufahamu kama mwanaume anafaa kuwa mumeo au anakupotezea muda - The Choice

Sifa 12 kuweza kufahamu kama mwanaume anafaa kuwa mumeo au anakupotezea muda

0

Wakati mwingine unaweza kuwa kwenye uhusiano na mtu ukaanza kujiuliza, hivi huyu atafaa kuwa mume wangu wa siku za usoni au ananipotezea muda?

Kuweza kutambua kama mtu anafaa kuwa mke au mume inatakiwa ufanya uchagunguzi wa kina na ukubaliane na matokeo. Hapa chini tunaeleza sifa chache za kuweza kutambua kama mtu anafaa kuwa mumeo au anakupotezea muda.

1. Mwanaume anayefaa kuwa mumeo atakuonyesha uimara wako na kukusaidia katika kila unachokifanya, lakini ukiona mtu hayuko hivyo, fahamu kuwa anakupotezea muda.

2. Mwanaume anayefaa kuwa mumeo atakuheshimu na kuheshimu uhusiano wenu, lakini mwingine atataka mle bata hajali sababu anajua siku si nyingi mtaachana.

3. Mwanaume anayekupenda na kutaka kuwa mumeo ataona mafanikio yako kama ya kwake pia, atapigana kila siku kuhakikisha unafanikiwa zaidi, lakini ukiangukia mikononi mwa tapeli atakula hadi mtaji wako.

wife-gives-husband-cheating-test-results-are-as-expected-5-photos-5

4. Mwanaume anayetaka kuwa mumeo atakuona kuwa wewe ndio mrembo na chaguo sahihi kwake, lakini wale vijana wa mjini wao kila siku atakuwa anatafuta makao mapya.

5. Ukiona mwanaume anakufanya unajiona uko salama, huyo anafaa kuwa mume, lakini ukiona upo kwenye uhusiano na mtu anakufanya hujiamini, anakupotezea muda.

6. Mwanaume anayetaka kuwa mumeo atahakikisha wewe kuwa na furaha ni jambo la msingi, lakini wale wapiga dili wanataka kutumiza haja zao wahangaike na mambo mengine.

african-american-man-woman-450rp0818081

7. Mwanaume anayetamani kila mara kuzungumza na wewe, majadiliane mambo yanayowahusu na jinsi ya kujiinua zaidi anafaaa kuwa mumeo, sio mtu kila ukiongea anakupigia kelele unyamaze au akiona simu yako akanasirika.

8. Anayefaa kuwa mume atakaa chini na wewe na kuweka mipango ya siku za mbeleni, kama kuna sehemu mnatakiwa kwenda au kitu cha kufanya, lakini ukikutana na wale wengine, yeye hana ratiba, anakurupuka tu kufanya mambo yake.

9. Mwanaume anayefaa kuwa mumeo atakufanya ujione kuwa wakati wote unahitajika, lakini mwingine utakuwa unajiona kama king’ang’anizi.

10. Mwanaume anayefaa kuwa mumeo atahakikisha kila mara anajua unaendeleaje na kujua kama tatizo au upo salama, lakini mwanaume wa mjini anaweza kukaa kimya hata siku mbili bila kukujulia hali.

vllkyt412nnrqgr5o-774fde0c

11. Anayefaa kuwa mumeo ni yule mwanaume ambaye hachoki kujifunza na kujua mambo zaidi kuhusu wewe. Lakini mwanaume anayekupotezea muda yeye hajali kukufahamu sababu anaona haina msaada kwake.

12. Mwanaume anayefaa kuwa mumeo ni yule anayetambua na kuiheshimu nafasi ya Mungu katika maisha yenu. Atahakikisha kila mara mnakwenda kusali, usiku mtasali pamoja kabla ya kulala na asubuhi kabla ya kuanza majukumu. Mwanaume anayekupotezea muda yeye akikurupuka asubuhi anatupa shuka na kukimbia na hakumbuki siku aliyoenda kanisani au msikitini.

Share.

About Author