Simba Kutupwa Nje Kombe la Shirikisho..!!! - The Choice

Simba Kutupwa Nje Kombe la Shirikisho..!!!

0
Klabu ya Simba huenda ikatupwa nje ya michuano ya kombe la shirikisho kufuatia kumpanga beki wake Novalt Lufunga kwenye mchezo walioshinda mabao 2-0 dhidi ya Polisi ya Dar es salaam huku akiwa na kadi nyekundu aliyoipata kwenye michuano iliyopita.
 Kwa mujibu wa rufaa ya klabu ya Polisi inadai kwamba Lufunga alilimwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa mwisho wa michuano hiyo msimu uliopita dhidi ya Coastal Union ya Tanga ambapo Simba ilitupwa nje ya mashindano.
 Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu’ ambaye amelitolea ufafanuzi suala hilo huku akikanusha kuwa Lufunga hakucheza mchezo uliofuata baada ya ule wa Coastal, lakini pia akasema kuwa kanuni za mashindano hayo ni tofauti na kanuni za ligi.
Facebook Comments
Share.

About Author