Simba Walipeleka Kombe la Azam FA Cup Bungeni Leo - The Choice

Simba Walipeleka Kombe la Azam FA Cup Bungeni Leo

0
Siku mbili baada ya klabu ya Simba kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho, imepata mwaliko bungeni.
Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbao FC ya jijini Mwanza, bao lililopatikana ndani ya dakika ngumu 120 katika mchezo uliopigwa jana Jumamosi makao makuu Dodoma kwenye Uwanja wa Jamhuri.
Kwa matokeo hayo, Simba imekata tiketi ya kupanda ndege na kuungana na watani zao Yanga. Simba watawakilisha Taifa katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF).
Pia, baada ya kupeleka kombe hilo bungeni, itakwenda Kondoa kwa ajili ya kucheza mchezo wa kirafiki na Kondoa Kombaini.
Baada ya kukamilisha ratiba hiyo, itasafiri kwa basi kurudi Dar es Salaam tayari kujiandaa na mashindano ya Ligi ya Sportpesa.
Share.

About Author