Spurs wawapunguzia kazi Leicester City - The Choice

Spurs wawapunguzia kazi Leicester City

0

Klabu ya Leicester City itashinda Ligi Kuu ya Uingereza Jumapili iwapo itafanikiwa kulaza miamba Manchester United uwanjani Old Trafford Jumapili.

Ushindi nyumbani kwa mabingwa hao mara 20 wa Uingereza utatosha kuwahakikishia taji baada ya Tottenham kutoka sare 1-1 na West Brom Jumatatu.

Mabao yote mawili yalifungwa na beki wa West Brom Craig Dawson, moja la kujifunga dakika ya 33 lakini baadaye alifidia kwa kufunga dakika ya 73.

Matokeo hayo yaliwaacha Spurs wakiwa alama saba nyuma ya Leicester, kila timu ikiwa imesalia na mechi tatu za kucheza.

Leicester City, chini ya meneja Claudio Ranieri, walianza msimu uwezekano wao wa kushinda ligi ukiwa 5,000-1.

Lakini Arsenal, Manchester City, Manchester United na mabingwa watetezi Chelsea, ambao kawaida ndio hupigania taji, wameshindwa kufana msimu huu.

Akiongea baada ya mechi hiyo ya Jumatatu, meneja wa West Brom Tony Pulis aliambia BBC Radio 5 kwamba: “Ninataka Leicester washinde. Leicester wana hadithi ya kusisimua na sidhani inaweza ikajirudia kwengineko ila hapa kwetu nchini.

418 total views, 2 views today

Facebook Comments
Share.

About Author