Tangazo la Arsenal mtandaoni laleta mzozo kuhusu Sanchez. - The Choice

Tangazo la Arsenal mtandaoni laleta mzozo kuhusu Sanchez.

0

sanche

Kuna msemo utakua umeshakutana nao kama wewe ni mtumiaji sana wa mtandao ambao unasema “Internet Got No Chill”. Maana yake ni kwamba watumiaji wa internet hawana mzaha au hawatulii hata kwa post ya kawaida basi hupenda kuikuza kwa mawazo yao iwe kubwa.

Sasa swala hili limeikuta Arsenal baada ya kutumia picha ya mchezaji wao Alexis Sanchez kwenye tangazo la punguzo la gharama ya baadhi ya bidhaa muda huu wa Christimas kwenye maduka yao.

Kama unavyoona tangazo hapo chini linaonyesha kwamba kuna punguzo hadi la asilimia 75 kwenye bidhaa za Arsenal. Modela wetu ni Sanchez kama unavyomuona.

Kutokana hali iliyopo sasa hivi watumiaji wa internet wameanza kutumia picha ile kuanzisha utani wa kwamba Arsenal wameshindwa kukubaliana na Sanchez na wameamua kumuuza kwa punguzo la asilimia 75.

Picha hii inashambaa mitandaoni na inakua mwimba kwa mashabiki wa Arsenal hasa pale linapokuja swala la utani.Mkataba wa Sanchez wa sasa hivi unategemea kuisha mwaka 2018, kama Arsenal wakishindwa kutimiza matakwa ya mchezaji huyu. Kuna uwezekano wa kujiunga na Chelsea

Share.

About Author