TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA 23.4.2017 - The Choice

TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA 23.4.2017

0

                            TETESI ZA USAJILI MANCHESTER CITY 23.4.2017

  • Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anatarajiwa kupewa mzigo wa Pauni milioni 250 kama pesa kwaajili ya Usajili kipindi dirisha la Usajili litakapofunguliwa majira ya Joto Barani Ulaya. The Sun wameandika kuwa Guardiola atatumia kiasi hiko kuwavuta Alexis Sanchez , Kyle Walker wa Spurs na Virgil van Dijk wa Southampton
  • Haijaishia kwa hao Tu wengine wanaotajwa kuwindwa na Guardiola ni Benjamin Mendy  tokea Monaco na Luke Show wa Manchester United
  • Licha ya Pep Guardiola Kukiri kumwitaji Sanchez bado Manchester United nao wamekuwa wakitajwa kumfatilia kwa ukaribu Sanchez ili kupata Saini Yake.

                       TETESI ZA USAJILI MANCHESTER UNITED 23.4.2017

  • Manchester United watamshughulikia matibabu yote Zlatan Ibrahimovic lakini hawataongeza mkataba naye Msimu utakapomalizika, Zlatan anamkataba wa mwaka MMOJA unaoisha mwishoni mwa msimu Huu.(Daily Mirror)
  • Manchester United watakubaliwa kumsajili straiker toka Juventus Andre Belotti endapo tu watakidhi kutoa mzigo wa pauni milioni 84 kama pesa ya Usajili (Mirror )
  • Boss wa Everton Ronald Koeman amemwambia Jose Mourinho aachane na mbio za kumfukuzia mchezaji Romelu Lukaku, United wamekuwa wakiandikwa mara kadha wa kadha kumfukuzia Lukaku.

                               TETESI ZA USAJILI ARSENAL 23.4.2017

  • Timu ya Arsenal toka jiji la London wametajwa na Daily Mirror kuwa wanamwania mchezaji wa Monaco Kylian Mbappe
  • Arsenal Pia wanamwangalia kwa ukaribu kiungo wa Udinise Jakub Jankto kwa dau la pauni milioni 6. Kupata habari zetu mapema zaidi
Share.

About Author