Uamuzi wa Yanga kuchagua uwanja wa Amaani kuwa uwanja wa nyumbani - The Choice

Uamuzi wa Yanga kuchagua uwanja wa Amaani kuwa uwanja wa nyumbani

0

3-4

Nina imani kubwa kuwa TFF kwa ushirikiano na ZFF watalikataa ama kulipinga hili kwa sababu kimsingi uwanja wa Amaan upo Zanzibar ambapo ligi yao inafanya kazi kwa kujitegemea na pia kwenye haki za fedha za Udhamini hii haikuwa imependekezwa kwa maana ya baadhi ya vilabu kutokuwa pia na bajeti ya kufika huko katika mwaka wa mahesabu wa kifedha wa kila klabu ambao hufungwa mapema baada ya maandalizi ya mahesabu ya mwaka mzima wa matumizi ya klabu husika.

Kwa hili hata vilabu vina haki ya kupinga hadharani. Sheria za ligi yoyote huitaji nadhani vilabu kuchezea michezo ya ligi katika zonal area inayotambulika na chama kinachoendesha ligi hiyo isipokuwa kwa issues za kuweka neutrality grounds, kuepuka fujo kwa maana ya kutokuwepo kwa football hooligans na vitu kama hivyo. Sidhani kama hii ni sababu ya Yanga kwa sababu hakuna maafa, hawajaomba kwa mchezo mmoja wa kuweka usawa “netrality” ili kuamua matokeo tatanishi ama yaliyolingana na sidhani kama TFF italipitisha hili.

Vilabu vya Wales wengi wanaweza kuchukulia mfano kama Cardiff na Swansea lakini hawajui kuwa timu hizi zinatambulika kuwepo kwenye mfumo ule wa Championship na Premier league na zinapanda daraja kama nyingine. Sheria ya Uingereza kwa vilabu vyake na vile vya visiwa vyake ni kuwa, zile zilizokuwa wanachama rasmi wa FA na zinazofanya kazi chini ya kanuni za ligi za PL pekee ndio zenye mamlaka ya kuhusika na ligi ile kwa namna yoyote na vilabu hivi vya Wales vimeandikishwa chini ya mwamvuli wa FA.

img_0174

Kuruhusu Yanga kucheza kule maana yake ZFA watakuwa wameruhusu ligi mbili tofauti katika eneo moja which means lazima iathiri muendelezo wa ligi ya kwao. And that’s to mean that Simba too wanaweza kuomba uwanja wa Mlandege (sijui kama bado upo, just to refer) ili watumie huko. So practically its a null idea and which doesn’t have to happen. Pia suala la udhamini, je Vodacom wataenda kuweka mabango yao kule Amaan? DTB bank pia?

Share.

About Author