Uongozi Simba watoa tamko ishu ya kina Kichuya na hatma ya Masoud Djuma - The Choice

Uongozi Simba watoa tamko ishu ya kina Kichuya na hatma ya Masoud Djuma

0

Kaimu Rais wa Simba atoa tamko kuwahusu kina Kichuya na Mkude,anena pia hatma ya Masoud Djuma baada ya Mapinduzi

Kaimu Rais wa Klabu ya Simba Salim Abdallah maarufu kama TRY AGAIN amesema wao kama viongozi wa klabu ya Simba watakaa na kutoa tamko kuhusu kitendo cha baadhi ya wachezaji wa Klabu ya Simba kuonekana kutokaa benchi mara baada ya kufanyiwa mabadiliko (Substitutions)

“Simba ni Taasisi kama kuna mchezaji, au kiongozi au mfanyakazi wa Simba ame- miss behave zipo taratibu za kufanya ndani ya uongozi tutachukua hatua kwa aina ya utovu wa nidhamu ambao umeonekana hakuna shaka watu watulie tu. ”

alisema Try Again

” Tutafanya uchunguzi tutaongea nao, tutaongea na kocha, tutaongea na team manager, tutaongea na wachezaji, tutaongea na Captain mwisho tutajua ni nini kilichotokea  “

Aliongezea Salim Abdallah

KUHUSU KOCHA MASOUD DJUMA

Kuhusu hatma ya Masoud Djuma Try Again amesema kuwa Masoud ni kocha msaidizi na wao kama Simba bado wanamtazama na kama akifanya vizuri uongozi wa Simba ni Uongozi ambao uko Flexible unaweza ukaamua chochote kwa wakati wowote ila kwasasa watu watulie wafanye kazi.

” Huyu ni mwalimu msaidizi, hayo yatakuja baadaye bado tupo kwenye mchakato tunamtazama nini cha kufanya kama atafanya vizuri basi viongozi wa Simba wako flexible  any time ni mapema tupeni muda tufanye kazi.”

Simba walijikuta wakitolewa hatua ya Makundi mara baada ya kushinda mchezo mmoja, kutoa sare moja na kufungwa michezo miwili hivyo kukosa sifa ya kuendelea mbele kwenye michuano ya Mapinduzi Cup 2018

3,814 total views, 2 views today

Facebook Comments
Share.

About Author