Uongozi wa Diamond Waahirisha Kuachia Wimbo wa Diomondi na Rick Ross - The Choice

Uongozi wa Diamond Waahirisha Kuachia Wimbo wa Diomondi na Rick Ross

0

Uongozi msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz umeahirisha kuachia wimbo mpya wa msanii huyo ‘Waka’ ambao amemshirikisha rapper kutoka nchini Marekani Rick Ross.

Akithibitisha hilo Meneja wa Diamond Platnumz, Sallam amesema kuwa kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao wimbo huo hauwezi kutoka leo Desemba mosi kama ilivyokuwa imepangwa awali.

“Tunaomba Msamaha Wimbo wa #Waka ulitakuwa kutoka siku ya leo kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu kwahiyo hautaweza kutoka leo lakini muda sio mrefu tutawajuza!! Sorry for any inconvenience“ameandika Sallam kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu Diamond Platnumz aliingia location kushoot video ya wimbo huo na Rick Ross huko nchini Marekani.

Share.

About Author