VIDEO: Magoli na rekodi 6 zilizowekwa baada ya ushindi wa Chelsea dhidi ya Arsenal - The Choice

VIDEO: Magoli na rekodi 6 zilizowekwa baada ya ushindi wa Chelsea dhidi ya Arsenal

0

Arsenal wamechezea kisago kingine kizuri cha magoli 3-1 kutoka kwa Chelsea kwenye game ya Premier League iliyopigwa kwenye uwanja wa Stamford Bridge.

Magoli ya Marcos Alonso, Eden Hazard na Cesc Fabregas yalitosha kulizamisha jahazi la Wenger ambao walipata bao la kufutia machozi dakika ya 90 likifungwa na Olivier Giroud.

Ushindi huo unaifanya Chelsea kuendelea kujikita kwenye kilele cha msimamo wa EPL baada ya kufikisha pointi 59 na kuweka tofauti ya pointi 12 dhidi ya Tottenham na Arsenal zenye pointi 47.

Rekodi sita zilizowekwa baada ya ushindi wa Cheslea 3-1 Arsenal

Chelsea imeshinda mechi tisa mfululizo za Premier League kwenye uwanja wao wa nyumbani huku ikiwa imefunga jumla ya magoli 24 na kuruhusu kufungwa magoli manne.
Arsenal imepoteza mechi nne kati ya tisa zilizopita za Premier League
Chelsea imeshinda mechi zote tisa za Premier League msimu huu ambazo Hazard alifanikiwa kufunga.
Petr Cech ameshindwa kutengeneza clean sheet kwenye mechi nne zilizopita za Premier League dhidi ya Chelsea akiwa Arsenal na ameruhusu magoli kwenye mechi zote alizocheza Stamford Bridge.
Diego Costa hajafunga mfululizo kwenye mechi za Premier League kwa mara ya kwanza tangu May 2, 2016 (mechi tatu mfululizo).
Cesc Fabregas amefunga goli lake la kwanza dhidi ya Arsenal kwenye mchezo wa Premier League.

 

Share.

About Author