Home News Vyuo 20 vilivyofutiwa usajiri na Serikali

Vyuo 20 vilivyofutiwa usajiri na Serikali

29
0

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE) limefuta usajili wa vyuo 20 kwa sababu mbalimbali ikiwemo kushindwa kufuata utaratibu wa usajili wa vyuo vya ufundi na upungufu wa rasilimali za kufundishia.

Pia, jumla ya vyuo 9 vimesitishiwa kudahili wanafunzi wapya kuanzia mwaka wa masomo 2018/2019 kwa kuzingatia kifungu cha 22(1) cha usajili wa vyuo vya ufundi

Aidha, NACTE imetoa agizo kwamba kabla ya kuanza kuendesha mafunzo ya kozi yoyete chuo kinatakiwa kihakikishe kuwa mtaala wa mafunzo hayo umepitishwa na Baraza na idara itakayosimamia mafunzo hayo

Kaimu Katibu Mtendaji wa NACTE, Dkt. Adolf Rutayuga amesema “Kuna vyuo ambavyo mapungufu yake yalikuwa ni makubwa kiasi kwamba tumevisitishia kutoa mafunzo na vyenyewe hivi ni vyuo 20, lakini kuna vyuo vingine ambavyo tumekuta vinaendesha Program ambazo hazina idhini ya Baraza”