Wachezaji 6 ambao nje ya soka ni wanamuziki - The Choice

Wachezaji 6 ambao nje ya soka ni wanamuziki

0
----mwisho-----

petr-cech

Mara kadhaa tumewaona wacheza soka wakicheza golf au tennis kama sehemu yao ya burudani au wawapo mapumzikoni huku wengine wakipenda kusikiliza muziki. Lakini baadhi yao wanafanya muziki serious hadi kufikia hatua ya kurekodi nyimbo.

Hapa kuna orodha ya baadhi ya wachezaji wanaojihusisha na muziki nje ya soka.

6. Wayne Rooney/ Ed Sheeran-muimbaji

rooney-singing

Anaweza  akawa hajaachia wimbo lakini baadhi tunafahamu Rooney anaweza kuimba. Ameonekana kwenye picha mara kadhaa akiimba pamoja na mwimbaji maarufu wa UK Ed Sheeran kwenye kumbi za starehe.

Amekuwa ni mhudhuriaji mzuri wa show za Ed Sheeran kila muda anapopata nafasi ya kufanya hivyo.

Tusubiri huenda siku moja Wayne Rooney akaachia single yake.

5. Ian Wright- Arsenal (mwimbaji)

ian-wright

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Ian Wright hakuwa akilijua goli tu, alifanya vyema pia hata kwenye upande wa muziki. Mwaka 1993 aliachia kibao chake kilichokwenda kwa jina la  “Do the right thing”.

Kijana wake Shaun-Wright-Phillips bado hajaingia studio hadi sasa, bado tunasubiri kuona pia kama atafata nyayo za baba yake

4. Glenn Hoddle and Chris Waddle-Tottenham Hotspur (mwimbaji)

glenn-hoddle-and-chris-waddle

Ma-star wa zamani wa Tottenham HotspurGlenn Hoddle pamoja na Chris Waddle waliachia wimbo wao ulioitwa “Diamond Lights” hiyo ilikuwa ni mwaka 1987. Wimbo huo ulifanya vyema na kushika namba 12 kwenye charts za UK.

Kitu cha kuvutia ni pale walipoa achia ngoma yao mpya saa chache kabla ya kusafiri kuelekea Ufaransa kukipiga dhidi ya Monaco.

3. Asamoah Gyan-Ghana

gyan-music

Tunaikumbuka ile penati aliyokosa kwenye kombe la dunia la mwaka 2010 kwenye mchezo wa robo fainali kati ya Ghana na Uruguay. Huyu jamaa aliyekosa ile penati ya dakika za lala salama pia ni mwanamuziki.

Alishiriki kwenye single inayokwenda kwa jina la African Girls. Asamoah Gyan alitumia jina la ‘Baby Jet’ kwenye wimbo huo alikumbana na ukosoaji hasa baada ya rafikiake kupotelea baharini kwa mazingira ya kutatanisha. Lakini Gyan hakuwa na cha kufanya kutokana na tukio la upoteaji wa rafikiake.

2. Andy Cole-Manchester United (Rapper)

cole-united

Striker wa zamani wa Manchester United Andy Cole hakuwa maarufu uwanjani pekee, alifanya hivyo hata kwenye upande wa muziki. Mwaka 1999 aliachia ngoma yake aliyoipa jina la “Outstanding”. Haikufanya vizuri sana lakini inawezekana isiwe ndio wimbo wake wa mwisho. Ngoja tusubiri huenda akarudi tena studio.

cole-n-yorke

Cole alifunga magoli 121 kwenye michezo 275 aliyoichezea Manchester United. Alishinda kila taji chini ya Sir Alex Ferguson.

1. Petr Cech-Arsenal (drummer)

cech

Golikipa No. 1  wa Arsenal Petr Cech huenda angependa kuzuia mikwaju yote inayoelekea langoni mwake akiwa pale Emirates lakini hawezi kuzuia mapenzi yake kwenye upigaji wa drums.

Ni mpiga drums kwenye band inayofahamika kwa jina la Eddie Stoilow.

cech-drums

Cech alishinda kila taji akiwa Chelsea kabla ya kuhamia Arsenal majira ya usajili ya msimu uliopita

Share.

About Author