Home Michezo Wachezaji hawa kupigwa panga Simba na Yanga

Wachezaji hawa kupigwa panga Simba na Yanga

249
0

Ligi kuu ya Vodacom inaelekea mwisho huku Simba ikiwa kileleni mwa ligi ikifwatiwa na Yanga .Simba imeshaondolewa kwenye michuano ya Kimataifa na tiketi pekee waliyobaki nayo ili mwakani waweze kushiriki michezo ya kimataifa ni kushinda taji la ligi kuu.

Endapo Yanga itashindwa kuchukua taji msimu huu na ikishindwa kutwaa taji la shirikisho basi Yanga mwakani hatutawaona kwenye mashindano ya kimataifa.

Kuna baadhi ya wachezaji katika vilabu hivi hawajafanya vizuri hivyo kupelekea kuweza kuondolewa katika vilabu vyao kwa msimu ujao.

Tukianza na Simba

Juma Luzio

Ni mchezaji ambaye hajawa na mafanikio na simba tokea afike na hata alipopata nafasi hakuonyesha makeke yake yaliyo tarajiwa hivyo kuwa na wakati mgumu wa kuweza kuendelea na Simba

Mwambeleko

Kusajiriwa kwa Asante kwasi aliyemfanya Muhamed hussein Tshabalala kukaa benchi ,dhahiri kabisa nafasi ya mwambeleko itakuwa finyu sana kuendelea na Timu kwa msimu ujao.

Ally Shomari

Ni mchezaji mzuri japo nafasi yake imekuwa finyu sana kutokana na kupona kwa Beki shomari Kapombe ambaye tokea apate nafasi amekuwa kwenye kiwango kizuri kinachopanda kila siku.

Mavugo

Yasemekana kutokana na kutokuwa na misimu mizuri ndani ya Simba ameona ni bora ajaribu sehemu nyingine huku Yanga wakionyesha nia ya kumchukua.Wakati Yanga wakiwa na nia ya kumchukua Simba wao hawana nia ya kuendelea naye msimu ujao

Mo Ibrahim

Habari za chini ya kapeti zinadai mchezaji Mo Ibrahi yuko mbioni kujiunga na Yanga msimu ujao.MO alisajiriwa na Simba akitokea Mtibwa Sugar hata hivyo hajawa na msimu mzuri katika Club ya Simba.Vyanzo ndani ya Yanga vinadai wanahakikisha kumalizana naye kabisa mwishoni mwa msimu.

Kwa upande wa Yanga

Chirwa

Habari zilizopatikana toka ndani ambazo sio nzuri kwa upande wa Yanga, Basi ni kitendo cha mchezaji wao Chirwa kusaini mkataba wa awali na Timu ya Diffa ElJadida ya Morocco.

Mpango mzima umefanywa na wakala wake ajulikanaye kama Taher khaleed

Mkataba wa awali aliosain na El jadida Chirwa kasaini mkataba wa miaka 3 .

Ngoma

Mchezaji wa kimataifa toka Zimbabwe Ngoma hataendelea na Timu yake hiyo kutokana na usumbufu mkubwa anaowaonyeshea Yanga.Ngoma amekuwa akiisumbua Yanga toka msimu wa kwanza huku akiwa anagoma kucheza hadi alipwe pesa zake na wakati mwingine akidai ni mgonjwa.Inaonekana Yanga washamchoka na hawana mpango naye tena na tusitegemee kumuona na Yanga kwa msimu ujao.

Tambwe

Tambwe ambaye alikuwa mkombozi mkubwa wa Yanga kwa msimu uliopita ,amekumbwa na matatizo ya kuumia mara kwa mara na huchukua mda mrefu kuweza kupona,Wengi wanasema umri ushamtupa mkono ndo maana kupona kwake huchukua mda mrefu

Mwashiuya

Kati ya Wachezaji ambao hawajaonyesha makeke kabisa katika msimu huu ukilinganisha na chipukizi kama Matrine pamoja na Yusuph mhilu ambao wameonyesha kiwango cha hali ya juu

Juma Mahadhi

Yaonyesha Juma Mahadhi anaipenda sana Yanga ila Yanga haimpendi Juma mahadhi hii ni kutokana na vitendo vyake vya kula bata sana wakati anasajiriwa na kusahau kazi yake iliyomleta Yanga.Sasa amekumbuka shuka kumekucha.

Youth Rostand

Ni golikipa aliyesajiriwa msimu huu akitokea African Lyon,lakini ameonyesha kuwa na mapungufu mengi sana katika eneo lake la ulinzi,hivyo kutokuwa na imani kabisa na wanayanga  na imani yao yote ikienda kwa Chipukizi Kabwili.