Wakala wa Ibrahimovic amalizana na Man United - The Choice

Wakala wa Ibrahimovic amalizana na Man United

0

Baada ya mshambuliaji wa PSG, Zlatan Ibrahimovic kuweka wazi kuwa ataondoka klabuni hapo baada ya msimu huu kukamilika na kuhusishwa a baadhi ya vilabu ikiwepo Manchester United, Arsenal na Chelsea, zimetoka taarifa kuwa Man United wao hawajatuma ofa kumtaka mchezaji huyo.

Akizungumza na Sky Sports News, wakala wa Ibrahimovic, Mino Raiola amekanusha taarifa hiyo na kuwa siyo sahihi Manchester United kuwa wametuma maombi ya kutaka kumsajili mteja wake.

“Katika hii dunia tunatambua kuwa waandishi wa habari wanaandika sawa na mitizamo yao, kuhusu jambo hilo siyo sahihi,

“Najua nini nitafanya mwaka ujao lakini siwezi kukwambia,” alisema Raiola

Share.

About Author