WCB Watembelewa na Waziri wa Mambo ya Ndani - The Choice

WCB Watembelewa na Waziri wa Mambo ya Ndani

0

Katika kile kinachoonekana viongozi wa serikali kuvutiwa na jinsi Diamond na lebel yake WCB wanavyoibadilisha tasnia ya muziki wa Tanzania kuwa fursa ya kibiashara na kazi rasmi, Mh. Waziri wa wizara mambo ya ndani, Mwigulu Lameck Nchemba ametembelea ofisi za WCB na kukutana na baadhi ya wafanyakazi na wasanii wa label hiyo ili kuwapa moyo na kuwahakikishia kuwa serikali ipo pamoja nao katika kuhakisha kazi zao zinalindwa kwa mujibu wa sheria. Pia kawaambia kuwa serikali haitasita kuwapa msaada pale watakapokwama na kuhitaji usaidizi wa serikali.

Binafsi nimeona ni jambo jema hasa ukizingitia wameshatembelea viongozi na mawaziri kadhaa. Rai yangu kwa wasanii wengine kuiga mfano wa WCB katika kuwa na ofisi maalumu na kuzipa thamani kazi zao.

Facebook Comments
Share.

About Author