YANGA JIANDAENI KUCHOMA JEZI NYINGINE - HAJI MANARA - The Choice

YANGA JIANDAENI KUCHOMA JEZI NYINGINE – HAJI MANARA

0

Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara (aliyefungiwa), amefungukia kitendo cha mashabiki wa Yanga kuchoma jezi ya mchezi wao kwa kusema hawana ustaarabu hata kidogo huku akiwapiga kijembe kwamba wajiandae kuchoma nyingine.

Manara amebainisha hayo kupitia mtandao wake wa kijamii siku moja kupita tokea kwa mashabiki kindaki ndaki wa klabu ya Yanga walioonekana wakichoma moto jezi aliyokuwa akivaa  Nahodha wao Haruna Niyonzima kabla ya kushindwana, kitendo kilichowatia hasira mashabiki hao.

“Katika miaka ya karibuni wachezaji kadhaa wa Simba walihamia Gongowazi hazikuchomwa moto jezi zao, wenzetu ustaarabu ziro ila wajiandae kuchoma nyingine ‘soon’ kama mlivyofanya mtafanyiwa ‘the same” aliandika Manara

Share.

About Author